Monday, September 28, 2015
Saturday, September 26, 2015
CCM Yarusha Jeshi La Anga Kuwakabili UKAWA Likiongozwa Na Mwigulu Nchemba.......Hapa Kuna Picha Wakipiga Push-Up Kumpa Sapoti Magufuli
Makada imara wa CCM Field Marshall Mwigulu Nchemba na Dkt. Hamis Kigwangalla waki-Magufulika kuonesha sapoti kwa Mgombea wao Dkt. John Pombe Magufuli aliyefanya tukio hilo siku si nyingi kwenye Jukwaa la Kampeni.
Field Marshall Mwigulu Nchemba akilakiwa kwa nderemo mjini Nzega
Friday, September 25, 2015
Wednesday, September 23, 2015
Tuesday, September 22, 2015
Emmanuel Mbasha Aachiwa Huru...Upande wa Mashtaka Umeshindwa Kuthibitisha kosa la Ubakaji dhidi yake
Mwimbaji
wa nyimbo za Injili nchini, Emmanual Mbasha (32), leo ameangua kilio
baada ya kuachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Ilala huku mke wake,
Flora amesema yuko tayari warudiane endapo ataomba radhi.
Mbasha alimwaga chozi muda mfupi baada ya kutoka katika chumba cha Mahakama alipopandishwa kizimbani kusomewa hukumu.
Mshtakiwa
huyo ameachiwa huru dhidi ya kesi ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili baada
ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha kosa.
Mwimbaji
huo ambaye kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo alionekana hana furaha,
alifikia uamuzi huo wa kulia mara tu baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo,
ambapo alipotoka nje ya chumba cha mahakama alipiga magoti chini huku
akiinua mikono juu na kulia kwa sauti huku akisema ‘mungu ni mwema’.
Mbasha
anakabiliwa na mashtaka mawili ya kumbaka shemeji yake mwenye umri wa
miaka 17 huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria
Kesi
hiyo namba 186 ya mwaka 2014, imeendeshwa kwa mwaka mmoja na miezi
miwili na kwa mara ya kwanza alifikishwa mahakamani hapo Juni 17 mwaka
2014.
Akisoma
hukumu hiyo leo, hakimu Mkazi Flora Mujaya alisema mahakama imemuachia
huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha kosa lililokuwa
likimkabili.
“Mahakama yangu imemuachia huru Mbasha baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha kosa ”alisema Hakimu Mujaya.
Hakimu
Mujaya alisema mahakama hiyo imetoa uamuzi huo baada ya kupitia
ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashtaka vikiwemo vielelezo
vilivyotolewa mahakamani hapo kama ushahidi.
Hukumu
hiyo, ilipaswa kutolewa wiki iliyopita , lakini iliahirishwa hadi leo
kwa sababu hakimu huyo ambaye ametoa hukumu hiyo leo alikuwa likizo .
Mke
wa Mbasha, Flora alisema yeye na familia yake wanaheshimu maamuzi
yaliyotolewa na Mahakama dhidi ya Mbasha na kwamba anaiomba familia yake
ikubaliane na maamuzi hayo na suala la kukata rufaa lisiwepo.
“Mimi
na familia yangu tunaheshimu uamuzi wa mahakama na ninaiomba familia
yangu ikubaliane na uamuzi huu uliotolewa na mahakama na suala la kukata
rufaa lisiwepo kwani uamuzi wa mwisho upo katika familia” alisema Frola
alipotafutwa kwa simu.
Wednesday, September 16, 2015
Diamond Platnumz apokea ushindi wa tuzo nyingine mbili

Headlines za Diamond Platnumz haziishii hapo, good news kwako mtu wangu msanii wetu wa Bongo Flava anazidi kuonyesha ubora wake kwenye nafasi mbalimbali za tuzo Africa… Diamond amepokea ushindi wa tuzo nyingine tena! African NAFCA Awards 2015 imemtaja Diamond kuwa Msanii wa mwaka anaependwa na wimbo wa ‘Nana’ umetajwa kuwa Wimbo wa mwaka unaopendwa!
Picha 5 kutoka ndani ya Studio ya Clouds FM wakati DJ Fetty anatangaza kuacha kazi ya utangazaji…
Jina lake ni Fatma Hassan aka DJ Fetty,
moja ya Watangazaji ambao wamepata majina makubwa sana TZ na East
Africa kutokana na kazi ya Utangazaji ambapo ana mchango mkubwa pia
kwenye muziki wa Bongo Fleva kama Mtangazaji wa show ya Entertainment, XXL ya Clouds FM.
September 15 2015 Show ya XXL inaandika Historia nyingine tofauti ambapo DJ Fetty ametangaza kuacha kazi ya Utangazaji na kuingiza nguvu yake zaidi kwenye masuala ya Biashara… wakati Fetty anatangaza hivyo, presenter mwingine pia Kened the Remedy ameungana na Timu ya XXL kwa mara ya kwanza
Ndani ya Studio ya Clouds FM, hapo yuko Kennedd, Adam Mchomvu, DJ Zero, B Dozen na DJ Fetty.
Tuesday, September 15, 2015
Adebayor aondoka Tottenham

Mshambuliaji wa kilabu ya Tottenham Emmanuel Adebayor ameondoka katika kilabu hiyo baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 31 kutoka Togo alikuwa hajaichezea Spurs
msimu huu na alikuwa amewachwa katika vikosi vya kucheza ligi ya
Uingereza pamoja na ile ya Yuropa.''Tunamuombea mema katika maisha yake ya baadaye',ilisema taarifa ya Tottenham.
Adebayor aliyewasili katika kilabu ya Manchester City kwa kitita cha pauni milioni 5 mwaka 2012,alikuwa amesalia na mwaka moja katika kandarasi yake na alikuwa akitaka kulipwa pauni milioni 5 ili kusitisha kandarasi hiyo mapema.
Hatahivyo kilabu ya Tottenham haijatangaza makubaliano ya usitishwaji wa kandarasi hiyo.
Akizungumza mapema juma hili ,kocha mkuu wa Tottenham Mauricio Pochettino alisema kuwa Adebayor hakuwa katika 'fikra zake' ama hata mpango wa mbeleni wa timu ya Tottenham.
Lori Lavamia Msafara wa Magufuli
MSAFARA
wa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli,
umenusurika kupata ajali, baada ya lori la mizigo kuuvamia na kugonga
magari matatu likiwamo lililokuwa limembeba mpiga debe wa chama hicho,
Amon Mpanju.
Ajali hiyo ilitokea jana asubuhi katika eneo la Njia Panda jirani kilomita chache kabla ya kuingia Maswa mjini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Gemin Mushi jana alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Alisema
wakati msafara huo ukitoka wilayani Meatu, askari polisi waliokuwa
wakiuongoza msafara huo walimuaru dereva wa lori hilo lenye namba za
usajili T 217 DDY kuegesha pembeni gari lake, lakini alikaidi.
“Msafara
wa mgombea urais ulikuwa jirani kuingia Maswa, dereva wa lori
aliamuriwa kuliweka pembeni akakaidi, tena kibaya akaongeza mwendo hali
iliyosababisha ajali.
“Lori
hili ni mali ya Kampuni ya Dilchadri Mill Ltd ya jijini Mwanza,
liligonga magari matatu likiwamo gari lenye namba za usajili T 217 CYM
aina ya Toyota Land Cruser ambayo iliharibika vibaya na kushindwa
kuendelea na safari.
“…Baada ya tukio hili, dereva amekimbia na polisi wanamsaka ili afikishwe mbele ya vyombo vya sheria,” alisema Kamanda Mushi.
Kutokana
na ajali hiyo, Kamanda Mushi amewataka madereva kuzingatia sheria za
usalama barabarani.Alisema hakuna mtu aliyeumia katika ajali hiyo.
Wakati huo huo, mgombea huyo aliendelea na mikutano yake katika wilaya za Maswa, Kishapu na Igunga.
Kwa
nyakati tofauti katika mikutano hiyo, Dk. John Magufuli, aliwataka
Watanzania kuchagua wabunge ambao watatetea masilahi yao badala ya wale
wanaotoka bungeni kila zinapowasilishwa bajeti.
Alisema endapo atachaguliwa anataka kuona Bunge linalotimiza wajibu wake, ikiwemo kupigania kero za waliowachagua.
“Haiwezekani wakati wa kujadili hoja za wananchi, wenzako wanatoka nje wanafanya hivi kwa kumkomoa nani?
“Maswa
ninyi ni mashahidi kwa muda mrefu hamkuwa na mtu wa kuwasemea tatizo la
maji, barabara na hata huduma za afya. Maana kila zinapopangwa bajeti
wao wanatoka nje je waziri atajuaje kama kuna tatizo eneo husika.
“Hii
si demokrasia hata kidogo ila ni kuwatesa wananchi, kwa hali hiyo sasa
Watanzania wote chagueni wabunge wenye masilahi kwenu na watakaosemea
shida zenu na si wale wanaotoka nje kila wakati (Ukawa),” alisema Dk. Magufuli
Aonya lugha chafu
Alisema ni vema viongozi wa vyama vya siasa kuepuka kampeni za matusi, kwani hazina tija kwa Taifa.
“Matusi
si hoja, ndiyo maana kila ninaposimama situkani mtu, najenga hoja.
Tunahitaji kujenga nchi yetu iwe ya amani siku zote,” alisema.
Friday, September 11, 2015
Kanisa Katoliki Sasa Kuvunja Ndoa
KIONGOZI
wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis jana alieleza mabadiliko mapya
yanayolenga kuwarahisishia Wakatoliki kuvunja ndoa zao na kuoa upya.
Dhamira
hiyo ni ishara nyingine ya dhamira ya Papa huyo kutaka kulifanya Kanisa
Katoliki liwe rafiki zaidi na kuendana matakwa ya walio wengi.
Akizungumza
kuhusu mabadiliko hayo, Papa alisema si haki kwa wenzi kuishi muda
mrefu ‘wakikandamizwa na wingu la shaka’ kuhusu uhalali wa ndoa zao.
Ikumbukwe
kwamba ni msimamo wa Papa kumkatalia Mfalme Henry the VIII wa Uingereza
kumtaliki mkewe Catherine wa Aragon katika karne ya 16 uliosababisha
England ijitenge na Rome na kushuhudia kuundwa kwa Kanisa la England
huku mfalme akiwa mlinzi wa Imani wa kanisa hilo.
Mabadiliko
makuu matatu aliyotangaza Papa jana ni kuondoa mchakato wa mapitio
ya mara ya pili wa uamuzi wa kutoa talaka kupitia mahakama ya kanisa
kabla ya ndoa kuvunjwa.
Mengine
ni kuwapatia maaskofu uwezo wa kuharakisha na kuvunja ndoa wenzi
wanapoamua wenyewe katika mazingira fulani kama vile ukatili katika ndoa
au uasherati na mchakato huo wa talaka kuwa bure, isipokuwa kwa kulipa
ada ndogo kwa ajili ya gharama za utawala.
Kabla
ya sheria hiyo, Wakatoliki waliotaka talaka walihitaji kibali kutoka
kwa mahakama mbili za kanisa, wakati sheria mpya inabakiza moja ingawa
rufaa bado zinaruhusiwa.
Kabla
ya sheria hiyo, wanandoa wa Wakatoliki wanaotalikiana bila idhini ya
kanisa na kuolewa upya walihesabiwa kama wazinifu na hawakuruhusiwa
kupokea komunio.
Lakini kwa mujibu wa utaratibu mpya, wanaotalikiana wakioa au kuolewa tena watabakia kuwa wafuasi wa kanisa hilo.
Mwaka
jana Papa aliunda tume ya wanasheria wa kanisa hilo kuboresha na
kurekebisha taratibu hizo kurahisisha wanandoa kuachana na kupunguza
gharama.
Mageuzi hayo yalikuja katika mfumo wa nyaraka mbili zinazoitwa ‘motu proprio’, neno la kilatini lililobuniwa na Papa mwenyewe.
Taratibu
hizo zitakuwa rasmi kama sehemu ya sheria za kanisa (canon law) ifikapo
Desemba 8 mwaka huu wakati Papa atakapoanza kutangaza Mwaka wa Jubilee
ambao kwa kawaida huhusishwa na msamaha.
Subscribe to:
Posts (Atom)






























