Friday, September 23, 2016
KAMA UMECHAGULIWA UDOM HII INAKUHUSU
Habari wana kwa wale ndugu zangu wa mwaka wa Kwanza mliochaguliwa katika chuo kikuu cha Dodoma. Kuna mambo ya kuanza kuzingatia mapema ili kuepusha utata pindi mtakapo anza kuripoti chuoni.
1-Kutoka stand ya mabasi Jamatini mpaka Chuoni nauli ni 400/= lakini kama utakua na Bag kubwa utalipia 500/= (Lakini Serikali ya Wanafunzi inaandaa utaratibu mzuri wa mapokezi kuanzia stand).USIPANDE TAX
2-Hakikisha umelipia malipo yoote yaani Tuition Fee, Direct Cost na Pesa ya Serikali ya Wanafunzi yaani UDOSO ambayo ni Tsh 5000/= Kufanya hivyo itakuepushia usumbufu siku ya kuripoti)
3-Malipo yoote yanalipwa Bank na kujua zaidi anza mazoea ya kutembelea Web Site ya Chuo yaani www.udom.ac.tz na www.udosochss.or.tz ambayo ni web ya serikali ya wanafunzi.)
4-Kwa wale wa Social Science and Humanities ukifika jamatini panda Coaster zilizo andikwa UDOM SOCIAL -BONDENI, wale wa course za Art watashukia kituo cha Social na wale wa Biashara na Lugha watashukia Bondeni-Kumbuka ukipanda gari tofauti na hizo itakula kwako.)
5-Pia kuna uwezekano wa kuripoti na kuanza registration ni Tarehe 12 mwezi wa 10 kwa wale wa College of Humanities and Social Science. Kama ratiba haita badilika, hivyo basi utaratibu unaandaliwa wa kuanza kupokea wanafunzi kuanzia 11 ambapo mtapewa sehemu za kulala kabla ya registration.
6-Kuwa makini na mizigo yako wizi upo kama kawaida woote mtakuwa wageni hivyo jaribu kuwa makini na kila umuonaye.
7-Kuhusu Hostel hapo msiwe na wasiwasi hata mkiripoti watu 5000 woote mtalala kwa raha zenu, chuo hakina matatizo ya Hostel kabisa.
8-Hakikisha unapesa ya kujikimu la si hivyo utajuta. Boom laweza kutoka baada ya week.
Mengine tutaendelea kujulisha hapa hapa, Pia kama unaswali ni vema ukauliza mapema.
Wale Continues wa UDOM karibuni kutoa msaada kwa ndugu zetu hawa 1st Year 2016-2017.
KWA USHAURI 0653546158
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment