Wapiganaji wa Kikurdi Kaskazini mwa Syria wanaripotiwa kuwatimua wapiganaji wa kundi la Islamic State kutoka mji wa Kobane.
Shirika
la haki za binadamu lenye makao yake nchini Uingereza lilisema kuwa
wapiganaji wa kurdi kwa mara nyingine wamechukua udhibiti wa mji wa
Kobane baada ya mapigano makali.Wanamgambo wa Islamic State walifanikiwa kuingia mji huo baada ya kufanya shambulizi la ghafla mapema siku ya Alhamis ambapo waliripotiwa kuwaua karibu watu 200 wakati wa uvamizi huo.
source; bbc.com
No comments:
Post a Comment