Tawi la kundi la Al Qaeda nchini
Yemen limethibitisha kuuawa kwa kiongozi wake wakati wa shambulizi la
ndege isiyokuwa na rubani ya Marekani
Ripoti kutoka kwa maafisa wa
usalama nchini Yemen zinasema kuwa Nasser al-Wuhayshi aliuawa siku ya
ijumaa katika mji wa bandari wa Mukala.Kundi lake limelaumiwa kwa kupanga mashambulizi kadha dhidi ya Marekani likiwemo jaribio la kuilipua ndege ya Marekani mwaka 2009, pamoja na shambulizi katika gazeti la Charlie Hebdo mji Paris nchini Ufaransa mwezi Januari mwaka huu.
No comments:
Post a Comment