Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, June 29, 2015

Ommy Dimpoz aoga mvua ya matusi mtandaoni


Mwanamuziki nchini Tanzania, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya kushambuliwa na mashabiki wake katika mtandao wa kijamii muda mfupi  baada ya kuweka picha ya tangazo la video mpya ya Ali Kiba, kuonyeshwa TRACE TV June 28 2015 kwa kile walichodai kuwa anamsaliti rafiki yake mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’.
 
Sambamba na hilo inadaiwa kuwa wanamuziki hao Ommy Dimpoz na Diamond, wana ugomvi wa chinichini ambao hawajataka watu kuufahamu na ndio maana mashabiki wamechukua hatua hiyo ya kumtukana na kumtolea maneno ya kashfa,
 
Kwa upande wa Ali Kiba, ameandika “Sasa ndugu zangu tukipost kuhusu Wasanii wenzetu mnatukana, tukikaa kimya tuna roho mbaya…. tufanyeje?? matusi tu hamjali kama watu wana wazazi unamtukania mzazi mwingine kafa, lakini kwa taarifa yenu hainiumi ng’o”.

No comments:

Post a Comment