Mahakama nchini Afrika Kusini imeahirisha kwa muda amri yake ya kumzuia rais wa Sudan Omar al Bashir, kuondoka nchini humo.
Mahakama
itasikiliza kesi hiyo tena Jumatatu ili kuamua ikiwa Bwana al-Bashir
atakabidhiwa kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC
kukabiliana na mashtaka ya uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari
yanayomkabili au la.
Rais huyo wa Sudan amekuwa nchini Afrika
kusini kuhudhuria kikao cha viongozi wa Umoja wa Afrika mjini
Johannesburg. Waziri wa mambo ya nje wa Sudan, Ibrahim al-Ghandour,
amesema Bwana al-Bashir atarejea Sudan baada ya mkutano huo. "Tupo hapa
kama wageni na kualikwa na serikali ya Afrika Kusini. Naamini serikali
ya Afrika Kusini itaweza kukabiliana na mahakama zake na yeyote
anayejaribu kumzuia Rais Bashir kuondoka nchini hapa. Naweza kuwaambia
Rais Bashir ataondoka kwa wakati kama ilivyokuwa imepangwa." anasema
waziri huyo wa mambo ya nje wa Sudan.
No comments:
Post a Comment