Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, July 3, 2015

AMUUA MWENZIE KWA KISU WAKIGOMBEA MWANAMKE

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Chacha Mwita (24) amekufa baada ya kuchomwa kisu na mwenzake wakigombea mwanamke.
Imeelezwa kuwa siku ya tukio marehemu akiwa kwenye baa moja mjini Sirari, nyakati za jioni kulitokea ugomvi kati yake na mtu mwingine ambaye hakufahamika jina wakigombania mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Dina. Wakati wa ugomvi huo, Mwita alichomwa kisu kifuani na aliyefanya kitendo hicho alitoroka ambapo majeruhi huyo alitokwa damu nyingi na alipofikishwa Hospitali ya Wilaya Tarime alifariki dunia.
Kwa upande wako, unaweza kuua mtu kwaajili ya mapenzi?

No comments:

Post a Comment