sayari
iitwayo Nibiru, ambayo kisayansi inafahamika kama Planet X ipo njiani
kuigonga dunia na hivyo kusababisha majanga mbalimbali kutokea.
ITAONEKANA ANGANI KAMA MWEZI
Kwa mujibu wa mitandao hiyo ya
kisayansi, sayari hiyo ambayo inaisogelea dunia kwa kasi kubwa,
itaonekana kubwa na angavu wakati wa usiku angani na kuwa katika umbo la
mwezi na hivyo kufanya miezi ionekane miwili. DALILI KWAMBA IPO JIRANI
Taarifa
zaidi za kisayansi zinasema kuwa, kadiri sayari hiyo inavyozidi
kusogea, dunia itaanza kutikisika na kusababisha matetemeko ya ardhi
kuongezeka sehemu mbalimbali. Mbali na dunia kutikisika na matetemeko,
milipuko ya volcano nayo itatokea huku idadi kubwa ya milipuko hiyo
mipya ikiongezeka, vimbunga vikubwa kama Tsunami vitaibuka na mwishowe
dunia itapigwa na bomu la miamba midogo na vimondo kutokea angani. DUNIA
ITAKUMBWA NA GIZA NENE
Wakati volcano zote duniani zitakapoanza
kulipuka na zingine mpya kujitokeza, dunia itafunikwa na giza nene na
matope kwa wakati wote wa usiku na mchana huku watu wakitakiwa kusoma
katika Biblia Joel 2: 1-2 na Zephaniah 1:14-17. NI TUKIO LA AINA YAKE
KARNE YA 21
Nibiru inatajwa kama kitu kinachoisogelea dunia
kinachoaminiwa kusababisha madhara makubwa ambapo kama hakitaigonga
dunia, kitasababisha mtikisiko usio wa kawaida kitakapopishana nayo.
Baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa kitendo hicho kitatokea mapema
katika karne ya 21 (tuliyonayo sasa). WANASAYANSI WAPINGANA
Baadhi ya
wanasayansi wanapinga kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wowote wa
kitafiti unaoonesha wazi kwa mabingwa wa anga za juu waliobobea wa
masuala ya nyota. MWANAMKE ALIWAHI KUOTA NDOTO
Kwa mara ya kwanza
jambo hilo lilitokea mwaka 1995, wakati mwanamama Nancy Lieder muasisi
wa mtandao wa ZetaTalk, aliwahi kudai kuoteshwa ndoto kwamba, Mei 2003
kuna kitu kitaingilia mfumo wa jua (solar system) na kusababisha dunia
kutoboka tundu litakalosambaratisha sehemu kubwa ya kizazi cha binadamu.
Lieder aliifafanua kuwa, kitu hicho kitakuwa na ukubwa wa mara nne ya
dunia. BAADA YA NDOTO
Baada ya mwanamama Lieder, mtu wa kwanza
kuizungumzia Nibiru alikuwa Mark Hazlewood, mwanachama wa zamani wa
mtandao wa ZetaTalk ambaye mwaka 2001 alichapisha kitabu kilichoitwa
Blindsided na kusema kuwa mwisho wa dunia ungekuwa mwaka 2003 baada ya
kuwasili kwa sayari ya kumi (Nibiru). Katika mfumo wa sasa, baadhi ya
wanasayansi wanasema sayari ziko 12, wakizitaja kwa namba 1. Jua 2.
Mercury 3. Venus 4. Dunia 5. Luna (mwezi) 6. Mars 7. Jupiter 8. Saturn
9. Uranus 10. Neptune 11. Pluto 12. Nibiru. IMANI NYINGINE YASEMA MWISHO
WA DUNIA NI FEBRUARI 22, 2014
Hata hivyo, utabiri mpya uliotolewa na
watu wa jamii ya Vikings jijini New York, Marekani umesema mwisho wa
dunia ni Februari 22, mwaka huu. Mitandao mbalimbali pamoja na gazeti
maarufu la Daily Mail la Uingereza lilielezea utabiri huo uliofanywa na
jamii hiyo ukidai kuwa mwisho wa dunia utatokana na Mungu Odin kupigana
na kuuawa na shetani Wolf Fenrir, hivyo kuiachia dunia
anayoishikilia.Wamesema baada ya kuiachia dunia itafurika maji ambayo
yatakuwa na sumu, hivyo viumbe wote watateketea. WATUMISHI WA MUNGU
TANZANIA
Baadhi ya watumishi wa Mungu nchini wamekuwa wakisimamia
andiko la kwenye Biblia linalosema kuwa, hakuna mwanadamu anayeijua siku
wala tarehe ya mwisho wa dunia na ni siri ya Muumba. Makanisa mengi
nchini Tanzania yana sera tofauti lakini yanaongozwa na Biblia moja.
Makanisa hayo ni Romani Katoliki, Lutheran (KKKT), Anglikana na makanisa
ya kiroho kama Full Gospel& Bible Fellowship la Zakaria Kakobe.
FREEMASON WABARIKI
Jamii ya Freemason tayari imebariki mwisho wa
dunia kwamba umefika na dunia inatarajie tukio kubwa la pamoja. Mitandao
ya jamii hiyo inataja kama hizi ni nyakati za mavuno kwa maana kwamba,
upande wa Mungu na shetani kushindania watu huku waendao upotevuni
wakiwa wengi. MFUMO WA DUNIA TANGU KUUMBWA
Kwa mujibu wa kitabu
kinachoitwa Panorama ya Biblia, ulimwengu tangu kuumbwa kwake umekuwa na
matukio makubwa kila baada ya miaka 2000 (inaweza isitimie au ikapita
kidogo). Tangu kuumbwa kwa Adamu na Eva mpaka gharika inadaiwa ni miaka
2000. Gharika hadi dunia kubadili mfumo wa mawasiliano (Mnara wa Babeli)
ni miaka 2000. Kuzaliwa kwa Yesu hadi saa ni miaka 2000 ambapo katika
karne hii, dunia huenda ikaingia katika tukio kubwa sana ambalo
halijawahi kutoke
No comments:
Post a Comment