Kama wewe ni msichana na umeshavuka miaka 30 bado hujaolewa na wala huna
mtu wa kueleweka ambaye amejitambulisha kwenu tambua kwamba una hali
mbaya.
Wasichana wengi siku hizi wamekua na tabia ya kupenda vitu
vya anasa hali inayopelekea sisi wanaume kuwaogopa kama ukoma.Mfano
kutaka kufanyiwa shopping za bei mbaya,kumiliki simu za gharama
zinazoanzia milioni moja na kuendelea,kupenda kuwa na mwanaume mwenye
mshahara unaoanzia milioni tatu kwa mwezi na kuendelea n.k
Hali
hii inasababisha hata sisi wenye kipata cha laki saba kushuka chini
tuwaogope kwa kuamimini kwamba hatuna uwezo wa kukidhi mahitaji yenu
hatimaye mnajikuta mnazeekea nyumbani kutaamakitaamaki miaka 45 hii hapa
ambapo ndo kipindi cha menopause kwa mwanamke yeyote.
Msipende
mteremko sababu hata huyo mwenye magari,majumba na kipato kikubwa hujui
ametumia njia gani mpaka kupata hivyo vitu.Starehe hazina mwisho hivyo
unapobweteka na starehe fahamu kwamba fainali uzeeni muda ndio refa
No comments:
Post a Comment