BIASHARA
ya ngono imeshamiri mkoani Dodoma wakati huu ambao vikao vya kumpata
mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) vimekwisha kuanza.
Uchunguzi
uliofanywa katika baadhi ya kumbi kama Club Maisha, Club Laazizi na
Matei Lounge, Chako ni Chako, umebaini kuwapo idadi kubwa ya kina dada
wakiwa wamevaa nusu uchi.
Katika
maeneo ya katikati ya mji wa Dodoma zilikuwapo hekaheka za wasichana
wanaojiuza ambao walionekana wakitafuta wateja bila ya wasiwasi wowote
na wengine walisikika wakisema wako kibiashara na siyo kuuza sura.
Eneo
maarufu la Chako ni Chako kuanzia jioni mpaka usiku kucha akina dada
hao wamekuwa wakijazana hadi kwenye taa za kuongozea magari huku
wakitafuta wateja wenye magari.
Baadhi yao ambao hawakutaka kutaja majina yao halisi mmoja wao alisema, ‘’Kaka sema una shilingi ngapi habari ya majina unataka kutupeleka wapi…?
‘’……wewe unaona shimo limetema hapa kila nikigeuka mwanaume na wanatoa ‘mpunga’ nadhani huyu rais ajaye atakuwa na neema.’’
Dada
mwingine ambaye aliyekuwa Dodoma Carnival karibu na Kituo Kikuu cha
Mabasi, alisema ametoka Arusha akiwa na marafiki zake kwa lengo la
kuwafuata wateja wa msimu walioko Dodoma.
Alisema
hadi sasa ana siku tatu akiwa Dodoma na tayari amekusanya zaidi ya
Sh 700,000 huku akiwatumia madalali ambao huwaunganisha kwa wateja
‘wazito’ (wenye fedha) kwa ujira maalum.
No comments:
Post a Comment