Muimbaji wa Marekani, Shaffer Chimere Smith maarufu kama Ne-Yo ameitaja
sababu iliyomfanya atake sana kukutana na Diamond Platnumz.
“Baada ya watu kusikia kuwa nilikuwa nakuja kwenye MAMAs jina pekee ambalo walikuwa wakilitaja kwangu ni Diamond Platnumz,” Ne-Yo alimwambia Vanessa Mdee kwenye interview ya MTV Base.
“Nikasema ni lazima nikutane na huyu jamaa, nahitaji kumuona,” aliongeza.
Siku
moja kabla ya tuzo hizo pia, Diamond alielezea jinsi Ne-Yo
alivyomtafuta. “Wakati nazungumza na D’banj @salaam_sk alinifata na
kuniambia @neyo anakutafuta anataka kukuona…” Ungependa kujua
kilichofata??? Kaa karibu na TV, Radio yaani Kiufupi Media zako Soon
utayaskia,” aliandika Diamond kwenye Instagram.
Ne-Yo na Diamond ni miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye MTV MAMA 2015.
No comments:
Post a Comment