Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, July 24, 2015

OBAMA AWASILI NCHINI KENYA CHEKI AKISALIMIANA NA NDUGUZAKE


Rais Barrack Obama wa Marekani, tayari amewasili mjini Nairobi.
Ndege iliyombeba rais obama ilitua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta muda mfupi baada ya saa mbili za usiku.
Alipowasili Rais Obama amelakiwa na mweyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.
mwendo wa saa mbili na robo rais Obama alitua ndege yake.
Alipowasili alizungumza kwa muda mfupi na mwenyeji wake rais Kenyatta na kisha kutia saini kitabu cha wageni kabla ya kuondoka.
Obama sasa ameandikisha historia ya kuwa rais wa kwanza wa Marekani, kuzuru Kenya akiwa ofisini.
Obama anatarajiwa kufungua mkutano wa sita wa kimataifa kuhusu ujasiri mali katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi.Mamilioni ya Wakenya wengine naowalifuatilia kuwasili kwake kwenye runinga.

No comments:

Post a Comment