Taarifa
kutoka Kiambu Kenya ambapo hisia tofauti zimetolewa kuhusiana na picha
ya askari wa kike wa usalama barabarani iliyofanya mabosi wake kumkemea.Sababu
kubwa ni picha ya Trafiki huyo aliyekua amevalia sketi fupi iliyombana
huku akiongoza doria wakati wa mashindano ya magari katika kaunti ya
kiambu ilisababisha picha iliyopigwa na mwanahabari wa gazeti moja
nchini Kenya kuzua mjadala kwenye mitandao ya kijamii Redioni na
Televisheni nchini Kenya.
Linda
Okello ni afisa wa trafiki mwenye cheo cha koplo aliitwa ofisini na
mkuu wa Trafiki kaunti ya kiambu James Mugeria na kumkemea vikali
akitaja kwamba vazi hilo linakiuka maantiki ya kikazi katika kikosi cha
polisi.
Baadhi
ya watu waliotoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii wamesema Trafiki
huyu alilengwa na wakuu wake bila kosa ikizingatiwa kwamba sare ama
magwanda ya maafisa wa polisi hutolewa kwao na serikali na pia kumekua
na madai kwamba Linda alikua amepewa uhamisho kaunti ya Mandera japo
maafisa wakuu wa polisi wemekanusha madai hayo.
Haya
yanajiri miezi kadhaa baada ya Naibu wa Inspekta mkuu wa polisi Grace
kaindi kuwaonya vikali maafisa wa kike wa polisi dhidi ya kutumia
lipstick, kuvalia mavazi ya kimtindo, bangili na vipuri virefu wakiwa
kazini.
Kifupi
taarifa kwa mafisa wa polisi iliyotolewa ilisema afisa yeyote
atakayepatikana na mavazi yaliyopigwa marufuku atakua amevunja sheria
Nambari 37 na sheria kwa maafisa wa polisi wa mwaka 2011 kipenge numbari
87-88 na atakabiliwa kisheria
No comments:
Post a Comment