Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, July 7, 2015

UKAWA WAJIONDOA RASMI BUNGENI


Umoja wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA leo umetangaza rasmi kususia vikao vya bunge vilivyobaki kwa madai ya kukiukwa kwa kanuni za bunge.
Akitangaza msimamo huo mjini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari, kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mh. Freeman Mbowe amesema wabunge wote kutoka katika vyama vinavyounda umoja huo hawataingia tena bungeni licha ya baadhi yao kuwa hawajaadhibiwa.
Wakati huo huo Bunge mchana huu limepitisha miswada miwili iliyokuwa imebaki baada ya mmoja kupitishwa jana.
miswada iliyopitishwa leo ni wa sheria ya usimamizi wa mapato yatokanayo na gesi na mafuta pamoja na muswada wa sheria ya uwazi na uwajibikaji katika uchimbaji bila ushiriki wa wabunge wa upinzani
Ingia hapa kwa taarifa zaidi, pamoja na kusikiliza alichokisema Tundu Lissu

No comments:

Post a Comment