Huku ulimwengu ukiadhimisha miaka 70
tangu ndege za kijeshi za Marekani ilipodondosha bomu la kinyuklia juu
ya Nagasaki tazama picha za janga hilo.
Ibada maalumu za ukumbusho
zinaendelea kufanywa katika mji wa Nagasaki, nchini Japan, kuadhimisha
miaka 70 tangu kulipuliwa kwa bomu ya atomiki jijini humo.Tarehe 9 Agosti mwaka wa 1945, ndege ya Marekani ikiwa imejihami kwa silaha zenye nguvu za kitonaradi ilidondosha bomu la pili kuwahi kutupwa katika uwanja wa kivita katika mji wa , Nagasaki ambao ulikuwa ndio kitovu cha uzalishaji wa viwanda nchini Japan.
Siku 6 tu baadaye Japan ilitangaza kuwa imejisalimisha katika vita hivyo vya dunia.
Takwimu zinasema kuwa takriban watu 74,000 waliangamia.
Hii ilikuwa ni idadi kubwa zaidi ya watu hususan ikitokea siku tatu tu
baada ya bomu la kwanza la kinyuklia kuua zaidi ya watu 140,000 mjini Hiroshima.
Bomu hiyo iliyotikisa na kuangamiza kabisa mji wa Nagasaki ilijulikana kwa jina la utani kama ''Fat Man''.
Ndege iliyotumika kutupa bomu hilo ilijulikana kama Bockscar, ilipaa kutoka kisiwa cha Mariana.
Rubani wake alikuwa Meja jenerali Charles Sweeney.
Inakisiwa kuwa zaidi ya watu 200,000 waliuawa katika milipuko hiyo miwili,
Wengine kufariki baadaye kutokana na miale ya sumu kutoka kwa mabomu hayo ya nguvu za kitonaradi.
Katika ibada ya ukumbusho iliyoandaliwa leo mjini Nagasaki,
wahasiriwa walimzomea waziri mkuu wa bwana Shinzo Abe kwa kutaka kubadilisha katiba ya taifa hilo ilikuwaruhusu wanajeshi wa Japan kuhusika na mapigano.
Meya wa mji wa Nagasaki naye alivutia waya huohuo akimkashifu waziri mkuu bwana Shinzo Abe kwa jitihada za kubadilisha katiba ya nchi.
No comments:
Post a Comment