Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, November 5, 2015

Dkt. Magufuli Aapishwa Rasmi Kuwa Rais wa Jamhuri Ya Muungano Tanzania

Hatimaye, Dkt. John Magufuli ameapishwa rasmi na kuwa Rais wa serikali ya awamu ya Tano ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania akihitimisha rasmi uongozi wa serikali ya awamu ya nne iliyoongozwa na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.
 
Rais Magufuli na makamu wake Bi. Samia Suluhu wamekula kiapo leo katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mbele ya viongozi wa nchi mbalimbali pamoja na viongozi wa chama, serikali na viongozi wa dini ambazo zilinogeshwa zaidi na gwaride la Jeshi la Wananchi.
 
Dkt. Magufuli ameapishwa na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Othman Chande na kupigiwa mizinga 21 ya heshima baada ya kukabidhiwa kijiti cha uongozi na rais wa serikali ya awamu ya nne, Jakaya Kikwete. 
 
Katika Jukwaa la Kiapo, walikuwepo Jaji Mkuu, Othman Chande, Katibu Mkuu Balozi Ombeni Sefue pamoja na Spika wa Bunge la 10, Bi. Anne Makinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 

No comments:

Post a Comment