.
Wikiendi iliyopita hitmaker wa Bado, Harmonize alimpeleka mpenzi wake
Jacqueline Wolper kwao Mtwara alikoenda kutumbuiza kwa mara ya kwanza
tangu aukwae ustaa kupitia label ya WCB.
“Time Ya Kumsaidia mama Harmo Kuanda Chakula Cha Usiku Mtwara Life
@wolperstylish,” aliandika Harmonize kwenye picha inayomuonesha Wolper
akichuma matembele shambani.
Naye Wolper alipost picha akiwa na mama mkwe na kuandika: I am having
the best time of my life.. Nikiwa na Mama angu… Kabla hamjatoka lazima
mpige story, akuchekeshe… Mjipikilishe.. Akushauri
Hapa nimepata rafiki kwa kweli…I love my mama Mkwe.. Mama Raj wangu.”
Wolper akiongea na mama yake Harmonize
Kwenye picha nyingine akiwa na mpenzi wake hiyo, Wolper aliandika:
Pale unapotoka kula ugali wa muhogo na sangara kwa mkwe yani ni amani tu…dizaini na ka rangi kamezidi kukubali.”
Uhusiano wa mastaa hao wawili umetengeneza vichwa vya habari mwezi huu baada ya kuamua kuuweka wazi.
No comments:
Post a Comment