Hatimaye imebainika kwamba Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, litafikia ukomo wake Julai 9, mwaka huu.
Hadi
kufikia mwisho wa uhai wake, Bunge hilo lililoongozwa na Spika Anne
Makinda (pichani), na Naibu Spika Job Ndugai, litakuwa limefanya
mikutano 20 huku vikao vya mwisho vikiwa ni 38.
Ratiba
ya nyongeza iliyotolewa jana na ofisi ya Bunge baada ya kikao cha
Kamati ya Uongozi, ilionyesha kuwa Rais Jakaya Kikwete atalivunja Bunge
hilo baada ya kulihutubia.
Pamoja
na tukio hilo la kihistoria, Bunge limejadili miswada mbalimbali
ikiwamo (iliyopitishwa) ya sheria ya fedha ya mwaka 2015, sheria ya
vituo vya pamoja mipakani ya mwaka 2015 na sheria ya kufuta sheria ya
benki ya Posta ya mwaka 2015.
Aidha,
baada ya maoni ya wadau wa habari, muswada wa haki ya kupata habari
ambao ulikuwa ujadiliwe Juni 27, mwaka huu, baada ya kusomwa kwa mara ya
kwanza, uliondolewa bungeni hadi serikali ijayo.
Miswada
inayoendelea kujadiliwa ni muswada wa sheria ya masoko ya bidhaa wa
mwaka 2015, muswada wa sheria ya kuwalinda watoa taarifa za uhalifu na
mashahidi wa mwaka 2015.
Mingine
ni muswada wa sheria ya Petroli wa mwaka 2015, muswada wa sheria ya
usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi wa mwaka 20q5, muswada wa sheria
ya uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji Tanzania ya mwaka
2015.
Ratiba hiyo imeonyesha kuwa muswada mwingine ni wa sheria ya Tume ya walimu wa mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment