Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, July 20, 2015

Baada ya Ushindi wa Tuzo, Diamond Atupa Dongo kwa Jokate........ Jokate Amwaga Machozi, asema Ipo Siku Mungu Atamuinua


Usiku wa jana kuamkia leo July 19 2015 Diamond Platnumz kanyanyua ushindi mwingine kwenye Tuzo za MTVMAMA2015, zilizokuwa zikitolewa Durban Africa Kusini.
 
Leo Diamond alipost Video inayomwonesha staa wa Mitindo Bongo, mrembo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ akicheza wimbo wa ‘Mdogomdogo‘ alafu akaandikia hivi; "Mbona Bado, Mtanyooka tu.." @ diamondplatnumz
 
Baadae Jokate nae akaandika kwenye ukurasa wake wa @Instagram kuhusu video hiyo ambayo alimpost Diamond.
 
"Tuki-support mtu ndio kama hivi matokeo yake mtu anatumia baadae kukudhalilisha. 
 
"Hii video aliyo-post kwanza ni TBT kama sijakosea mwaka jana mwishoni nilikuwa sehemu na my friends @bikira_wa_kisukumaakani-record na kumtumia@diamondplatnumz bila mimi kujua.
 
"Kiukweli sijui kwanini walifanya hivyo. Nikaja kujua baadae sana na nikaona sio big deal cause kila mtu anapenda mziki na sio dhambi kucheza mziki wowote uupendao.
 
"Ila kitendo cha@diamondplatnumz kwenda kuitafuta huko ilikokuwa hii video clip na kui-post leo najiuliza maswali mengi

"1, anataka ionekana kama nilikuwa nashangilia ushindi wake? Which is not bad hakuna ubaya hapo kama unaamini ushindi wake ni sifa kwa taifa ila

"2, Kwanini a-post na caption ya Na Bado Mtanyooka? Ili amkomoe nani? Au kwasababu niko karibu saaana na @alikibaofficialanatafuta kutuchonganisha? Ili iweje? Mimi I believe life goes on na kila mtu ana uhuru wa kumpenda au kuwa karibu na yule apendaye na kum-support ndio maana hata mimi nimekuacha na your new life

"3, Pengine ni kweli anaendeleza zile hulka zake za kudhalilisha wanawake aliokuwa nao waonekane sio kitu just because hawako na diamond platnumz chibu dangote. Which to me is just dead wrong.
 
"@diamondplatnumz hizi sio tabia tunazozitegemea kwa mtu anayejisema anakomboa mziki wa Tanzania sio kwa kuweka visasi na fitna zako wazi wazi hivi. Unatu fanya tukose imani nawewe zaidi na tunaogopa ku-support cause hukawi kutugeuka.
 
"Kuwa tofauti basi, onyesha mfano kwamba kweli hupendi beef unapenda mziki wa Tanzania uendelee ila kwa ulichoki-post unaonyesha wazi UNA visirani na hutaki mema unatafuta drama, kiki, vurugu unataka kila siku uwe wewe tu ambazo kiukweli mimi binafsi siziwezi utaendelea kushinda wewe tu katika hilo na sitashindana nawewe katika hilo kwasababu siwezi nawewe unajua kama ulivyoniimba mimi mpole, sinaga maneno ( ila kwenye kazi ndio nakuwa mkali kama pilipili ). Ila ungetumia busara kidogo.
 
"Just move ON kiroho safi. Naomba pia nitumie fursa hii kukupongeza kwa tuzo yako ya MTV ila@babutale hata wewe ndugu yangu? Is this how tunaendeleza so called uzalendo?
 
"Inshallah Kheri lakini yote maisha wanyonge sisi iko siku Mungu atatunyanyua.

No comments:

Post a Comment