Mkoa wa geita na viunga vyake jana ulizizima kwa muda wakati mgombea wa kiti cha urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dk.John Pombe Magufuli alipokuwa akitambulishwa na kuagwa na wapigakura wake wa jimbo la Geita huku wananchi wakimtaja kama mkombozi wa kulivusha taifa kuelekea katika haki na usawa kwa watanzania wote.
Akiwa
njiani kutokea mkoani mwanza kuelekea mkoani Geita katika eneo la
chato alikozaliwa msafara wa dr magufuli ulijikuta ukisimamishwa njiani
mara kwa mara na umati mkubwa wa wananchi bila ya kujali jinsia na rika
waliojitokeza barabarani kwa lengo la kutaka kumuona huku wakiwa na
matawi ya miti.
Akitambulishwa
na umati mkubwa wa wananchi katika ofisi za mkoa wa chama hicho
mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma Kasheku alisema chama
hicho hakika hakikukosea kumteua Dr. Magufuli kugombea nafasi ya urais
kupitia chama hicho kwa kuwa ni kipenzi cha watanzania wote bila ya
kujali itikadi za kivyama.
Akizungumza
wakati akiwashukuru,kuwaaga na kujitambulisha kwa wananchi
waliokusanyika katika ofisi za chama cha mapinduzi mkoani Geita na
hatimae vunja jungu katika jimbo la chato, mgombea urais wa CCM Dr.John
Pombe Magufuli alikishukuru chama hicho kwa kumuamini na kuongeza kuwa
makundi ya wagombea wa nafasi ya urais ndani ya chama hicho yamezikwa
rasmi na limebaki kundi moja la umoja ni ushindi.
Wakizungumzia
uteuzi wa Dr.Magufuli kugombea kiti hicho cha urais kupitia chama cha
mapinduzi baadhi ya wananchi walisema tanzania imepata kiongozi
atakayesaidia kuipeleka tanzania katika nchi ya ahadi.
Mgombea
Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe
Magufuli akiwahutubia maelfu ya Wanaccm na Wananchi wa Mkoa wa Geita.
Msafara
wa Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John
Pombe Magufuli ukiwasili kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Geita
No comments:
Post a Comment