soko la Tanzania limekuwa likipokea
bidhaa kutoka ndani na nje ya nchi lakini baadhi ya bidhaa zinaarifiwa
kuuzwa madukani huku zikikosa nembo za ubora.
Baadhi ya bidhaa hizo pia zimeonekana kuuzwa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Katika
maonyesho kama hayo ya biashara ya saba saba nchini Tanzania huwa ni
fursa ya wafanyibiashara na wajasiriamali kuonyesha bidhaa zao mbali
mbali lakini kwa wengine huwa wanatumia fursa hiyo kusambaza na kuuza
bidhaa duni kwa bei ya kutupa.
katika maonyesho hayo bidhaa hizo na nyingine zinaendelea kuuzwa huku kukiwa na sheria na utaratibu kamili .
Bi
Roida Andusamile ni msemaji wa shirika la viwango Tanzania na anasema
hali halisi ni kwamba kuna baadhi ya wajasiriamali ambao wanaonyesha
biashara zao wakati bidhaa zao hazijathibitishwa na shirika la viwango
kuwa zina ubora.
Hata hivyo viongozi wa maonyesho hayo
wanasisitiza kuwa wameweka uthibiti wa kutosha ili kukinzana na tatizo
hili la bidhaa feki katika maonyesho hayo ya biashara.
Ingawa baadhi ya wafanya bishara wanakiri kukosa kiambishi cha
kuonyesha ubora wa bidhaa zao zinawanyima soko , sio nyumbani tu lakini
hata kimataifa kwa kuwa uwezo wao bado ni mdogo ingawa bidhaa zao zina
ubora.
Wakati maonyesho hayo yakiendelea, maafisa wa serikali
wanachukua fursa ya kuwepo kwenye maonyesho na kutoa mafunzo kuhusu
ubora wa bidhaa .
Mamlaka ya chakula na dawa inasema iko makini
katika hilo kwani maafisa wao bado hutembelea mabanda ili kubaini bidhaa
feki zilizoingia.
Afisa wa uelimishaji jamii;James Ndege anasema
sio vyema kuwalaumu wafanyabiashara pekee yao kutokana na tatizo hili
kwani tatizo la bidhaa feki linamgusa kila mmoja.
Hata hivyo bidhaa hizi zisizo na viwango zimekuwa ni changamoto kwa kuwa na athari nyingi kiafya na usimamizi wake kuwa mgumu.
No comments:
Post a Comment