Kampuni ya Samsung imezindua simu yake nyembamba zaidi aina ya smartphone kufikia sasa.
Simu
hiyo kwa jina Galaxy A8 ina upana wa milimita 5.9 ikiwa ni wembamba wa
asilimia 85 ikilinganishwa na simu ya Galaxy S6 Edge.Licha ya wembamba huo waandisi wameweza kuiweka betri pamoja na kamera yenye uwezo wa mega pikseli 16.
Mmoja ya wataalam aliuliza swali la muhimu wa kutengeza simu nyembamba.
Kwa sasa Samsung imetangaza kwamba simu hiyo itauzwa nchini Uchina na Singapore.
''Galaxy A8 haitauzwa nchini Uingereza'' alisema msemaji wake.
Ijapokuwa itakuwa simu nyembamba zaidi kutoka kwa mojwapo ya kampuni kubwa ,kampuni nyengine za Uchina tayari zimeanza kuuza simu kama hizo.
No comments:
Post a Comment