Mke wa
mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli, Janeth Pombe. KUMEKUCHA! Siku chache baada ya Waziri wa
Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kuwa mgombea urais kupitia chama hicho, mkewe, Janeth Pombe
amechambuliwa vilivyo na walimu wenzake, Amani lina kila kitu.
Juzi,
Amani lilifika Shule ya Msingi Mbuyuni, Oysterbay jijini Dar ambayo
Janeth amekuwa akifundisha na kufanikiwa kuzungumza na mwalimu mkuu wa
shule hiyo na walimu wengine.
MWALIMU MKUU AANZA
Akizungumza na gazeti hili, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Doroth Malecela (John Malecela anamwita baba mdogo) alisema:
“Kwetu sisi kama shule, tunajivunia kwa sababu hata mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, mama Salma Kikwete alifundisha shule hii.
AOMBA MAGUFULI ASHINDE
“Kama
John Magufuli atafanikiwa kuingia madarakani, taifa linatakiwa kujua
Mbuyuni ndiyo shule inayotoa marais wetu kupitia wake zao.
“Hivi sasa
tunaomba uchaguzi uende vizuri, Magufuli ashinde ili naye tumlee. Mbali
na yote, lakini pia kuondoka Janeth kutatuachia pengo kwetu maana
tulikuwa naye kwa kipindi chote lakini ni wazi kwamba kama mumewe
atashinda urais, kisheria yeye Janeth hataweza kuendelea kufundisha tena
hapa,” alisema mkuu huyo wa shule.
MAISHA BINAFSI
Mwalimu
Doroth alimchambua Janeth Pombe (jina analotumia) kuwa, katika
mazingira ya shuleni, mwalimu huyo aliishi kama walimu wengine na si
kama mke wa waziri kwa sababu hajikwezi. Hata mavazi yake ni simpo tu.
“Kwanza
Janeth ni mcheshi, lakini pia ni mpole na mchapakazi. Ni mtu wa
kujichanganya na wengine kwenye shida na raha. Kwenye furaha hakusita
kuonesha uchangamfu wake hata kwa kucheza. Kila mmoja alipenda uwepo
wake,” alisema mwalimu huyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni ya jijini Dar. MASOMO ANAYOFUNDISHA
“Hapa anafundisha wanafunzi wa darasa la tano masomo ya Uraia, Historia na Jiografia.”
KUHUSU UCHELEWAJI
“Hapana,
kwa kufuata taratibu za kazi na sheria za shule, mwalimu Janeth alikuwa
akifika mapema na kuanza majukumu yake bila kupoteza muda.”
USAFIRI ANAOUTUMIA
“Amekuwa
akiletwa kazini muda mwafaka na gari na dereva wake na muda wa kutoka
pia alifuatwa kwa gari bila aina yoyote ya mbwembwe.”
Kibao cha Shule ya Msingi Mbuyuni. HAKUWA MTORO?
“Inapotokea
ana udhuru wa kumfanya ashindwe kuhudhuria shuleni amekuwa akitoa
taarifa mapema kwa uongozi. Kifupi alikuwa mtiifu, hakuringia cheo cha
mumewe hata siku moja na haikuwa rahisi mtu kumjua kuwa ni mke wa Waziri
John Magufuli bila kuambiwa.
KUHUSU FAMILIA
“Pamoja na kuwa
mume wake ni waziri, watoto wao wote wamesoma katika shule hii. Kuanzia
darasa la kwanza mpaka la saba na walikuwa wakishirikiana na wanafunzi
wenzao.
“Mtoto wao wa mwisho alimaliza hapa mwaka jana, sasa anasoma
Shule ya Sekondari ya Kata ya Oysterbay na kuna muda huwa anakuja
kutusalimia,” alisema mwalimu mkuu huyo.
SHEMEJI UNATUACHAJE
“Kuna
kipindi walimu tulisema JK unatuachaje shemeji yetu (kwa ajili ya mama
Salma), lakini alitujibu atakuja shemeji yenu mwingine. Kwa usemi ule
sasa tunaamini, shemeji yetu anaweza kupatikana tena.”
SIRI YA SHULE
Akieleza sababu inayoifanya shule yao kuibua wake wa marais (kama Magufuli atashinda) mwalimu huyo alisema:
“Hakuna
siri kubwa, huku Oysterbay, Masaki ndo’ wanakoishi vigogo wa serikali
hivyo huwa ni rais wake zao kufundisha kwenye shule hii.”
ANAIJUA SIASA?
“Mama Magufuli yeye mara kwa mara husifia kazi yake ya ualimu, sikuwahi kumsikia akisema anapenda siasa hayupo huko kabisa.”
No comments:
Post a Comment