Mwanamuziki wa chapa ya Pop, Rihanna ametibua mjadala mkali sana kwenye mitandao ya habari za Muziki na wasanii.
Hii
ni baada ya kipusa huyo kuachia video yake mpya ya dakika 7 siku tano
zilizopita ambayo inapongezwa kwa usanii na vilevile inakashifiwa sana
kwa kuonyesha viungo vya utu uzima na kuwa na fujo kupita kiasi.Aidha wanaoikashifu wanadai kuwa inaonesha unyama na ukatili wake ambayo wanahofu itawapotosha wafuasi wake wanaomtazamia kuwapa mwelekeo.Katika video hiyo Rihana anaonekana akimlewesha mwanamke ambaye mumewe inakisiwa anadeni lake.
No comments:
Post a Comment