Aliyekuwa Mbunge wa Muleba Kusini, Prof Anna Tibaijuka anayewania
jimbo hilo kwa mara ya pili, jana alishushwa jukwaani kwa kuzomewa na
wananchi wake katika kata ya Nshamba wilayani Muleba. Prof Tibaijuka
alishushwa jana wakati wa kampeni za kura za maoni kupitia CCM. Hali ya
kuzomewa ilidumu kwa dakika kadhaa jambo lililofanya Wagombea hao
kulazimika kuondoka. Kwa mara ya kwanza alizomewa juni 8, wakati wa
ziara ya kati
bu mkuu wa CCM Abdulrahman
Kinana katika kata hiyo hiyo. Akiwa na Kinana wananchi walimtuhumu
ufisadi wa fedha za Escrow na kushindwa kutekeleza ahadi ya kuwajengea
barabara ya lami.
Source: Mwananchi
Nini maoni yako kuhusu hilo?
No comments:
Post a Comment