Mji muhimu wa mwisho uliokuwa
mikononi mwa kundi la Al Shabaab kusini magharibi mwa Somalia wa
Baardheere umechukuliwa tena na vikosi vya Muungano wa Afrika (AU)
-miaka 7 baada ya wapiganaji hao wenye itikadi kali kuingia kwa mara ya
kwanza katika mji huo .
Wakazi wa mji huo wamesema vikosi vya
Kenya na Somalia vikiwa na silaha nzito na usaidizi wa mashambulizi ya
anga viliuvamia mji huo , ambao wapiganaji wa Al Shabaab waliutoroka
usiku.Vikosi vya AU nchini Somalia, na vile vya jeshi la Somalia, vilifanikiwa kuuteka mji huo baada ya mashambulizi makali. Majeshi kutoka Kenya, Somalia na Ethiopia yamekua yakiendesha harakati za kuuteka mji wa Baadheere kwa siku chache zilizopita.
Kumekuwa na mapigano makali viungani mwa mji huo, lakini wanamgambo wa Alshaabab walisalim amri na kuukimbia ,na hivyo kutoa fursa ya mji huo kuchukuliwa bila mapigano .
Wakazi wanasema kamanda mmoja wa Somali na vyombo vya habari vinavyounga mkono Al Shabaab wamethibitisha kuchukuliwa kwa mji huo.
Harakati hizo za kuuteka mji wa Baadheere zimefanikiwa siku chache kabla rais wa Marekani Barack Obama kufanya ziara Afrika mashariki ambapo suala la usalama nchini Somalia litakuwa kwenye ajenda kuu za ziara yake .
Kundi la Al shaabab lina uhusiano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda linapigana dhidi ya serikali ya Somalia kwa ajili ya udhibiti wa nchi hiyo.
Wiki iliyopita mashambulizi ya ndege zisizokua na rubani (drone) zilizoshambulia ziliripotiwa kuwauwa makamanda wa ngazi ya juu wa Al Shabaab.
No comments:
Post a Comment