Staa wa Bongo Fleva ambaye jina lake limebeba uzito mkubwa Afrika, Diamond Platnumz amepata mtoto wa kike toka kwa mpenzi wake Zari Hassani.
Mtoto huyo ameingia duniani saa 10 na dakika 40 Alfajir, Alhamis hii.
Haijaweza kufahamika kwa mara moja ni hospitali gani mtoto huyo
amezaliwa kwa kile meneja alichosema ‘usalama wa mama na mtoto’ kwakuwa
bado wapo hospitali.
“Sura ya mama yangu inatosha kueleza ni kiasi gani najiskia ndani ya
Moyo wangu, karibu kwenye ulimwengu @princess_tiffah,” ameandika Diamond
kwenye picha hiyo juu aliyoiweka Instagram.
Awali Diamond alisema kuwa Zari angejifungulia Tanzania.
No comments:
Post a Comment