Mwenyekiti wa chama cha Chadema Freeman Mbowe leo amesema kwamba chama cha Chadema kimempumzisha katibu mkuu wake Dk. Wilbroad Slaa kwa muda usiojulikana.
Akizungumza
katika mkutano wa baraza kuu Chadema Mbowe amesema kwamba chama cha
Chadema kimekubaliana kumpumzisha Dr. slaa kwa muda lakini nafasi yake
ya katibu mkuu katika chama hicho iko pale pale.
“Tumekubaliana
kwamba katibu mkuu Dr. Slaa apumzike kwa muda na sisi tuendelee
atakapokuwa tayari ataungana na sisi mbele ya safari, chama hiki
hakiendeshwi kwa siri tunakiendesha kwa mikakati” Amesema Mbowe
Ameongeza
kuwa Chadema hakiwezi kuwa chama cha kuhubiri mabaya ya jana na
kushindwa kuhubiri maendeleo ya kesho na kipigo wanachokipata CCM
hawajawahi kukipata tangu nchi imeanza vyama vingi vya siasa.
Hivi
karibuni kumekuwa na habari ambazo hazijathibitishwa zinazodai kwamba
Dr.Slaa ni mmoja kati ya wanasiasa wasiokubaliana na Mbunge wa Monduli
Edward Lowassa kuhamia katika chama hicho suala linalopelekea kuto
onekana katika vikao mbalimbali vya chama hicho vinavyo endelea jijini
Dar es salaam.
Katika
hatua nyingine Umoja wa katiba ya wananchi Ukawa unatarajia kumtangaza
mgombea wake wa urais ambaye ni Mbunge wa Monduli Edward Lowassa
aliyechukua fomu ya kuomba ridhaa ndani ya chama cha CHADEMA
No comments:
Post a Comment