Akizungumza
na Wanachama wa CCM leo katika ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba
jijini Dar es salaam mara baada ya mgombea wake wa Urais Dk.John Pombe
Magufuli kuchukua fomu ya kugombea urais tume ya Taifa ya Uchaguzi
amesema kwamba chama hicho kwa bahati nzuri mwaka huu kinashindana na
makapi yake ambayo kamwe hayawezi kuishinda CCM.
“Nchi yetu inakwenda kwenye uchaguzi ikiwa na wagombea na makapi, sasa kati ya mgombea na makapi nani mshindi?” Amehoji Kinana
Ameongeza kuwa kila mwanachama akitengwa na CCM mahala pake ni wapi? Huku mamia ya wananchi wakijibu ‘Chadema’ kwa sauti ya juu.
Naye
Mwenyekiti wa CCM Dk. Jakaya Kikwete amesema kwamba serikali ya CCM
imefanya mambo mengi ya Maendeleo na mwaka huu wana waahidi watanzania
ushindi wa kishindo.
Kwa
upande wa Mgombea Urais wa CCM Dk. John Magufuli amesema kwamba ikiwa
atachaguliwa kuwa rais anakwenda kufanya wananchi walicho mtuma kwa
kuwa shida za watanzania anazifahamu huku akirejea kauli yake Maendeleo
hayana chama.
Hivi
karibuni chama cha Mapinduzi kimepata mtikisiko mkubwa kufuatia
wanachama wake kuhama chama hicho na kutimkia Upinzani hususani Chama
cha Chadema akiwemo Waziri mkuu wa Zamani Edward Lowassa, Makongoro
Mahanga, James Lembeli pamoja na Ester Bulaya.
No comments:
Post a Comment