December 2014 baada ya shindano la Miss Tanzania kukamilika liliingia
kwenye headlines baada ya Baraza la sanaa la Taifa kutangaza kulifungia
shindano hilo kwa miaka miwili baada ya kujiridhisha kwamba limekiuka
taratibu lakini leo August 17 2015 Miss Tanzania imeingia tena kwenye
headlines baada ya Basata kutoa msamaha.
Hii hapa chini ndio taarifa iliyotolewa na BASATA.
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) limelifungulia shindano la urembo la Miss
Tanzania baada ya mwandaaji wake Kampuni ya LINO International Agency
Limited kufuata taratibu, kuomba radhi na kuyafanyia kazi baadhi ya
mapungufu yaliyojitokeza na kutekeleza masharti aliyopewa.
Itakumbukwa
kuwa mnano tarehe 22/12/2014 BASATA liliwaandikia barua LINO
International Agency Limited ya kulisimamisha shindano la Miss Tanzania
kwa miaka miwili (Mwaka 2015 na 2016) na kuwaagiza kujipanga upya na
kurekebisha kasoro ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara.
Mapungufu
yaliyobainishwa ni pamoja na; mosi, kutokufuata Sheria, Kanuni na
Taratibu za uendeshaji matukio ya Sanaa nchini, pili kutokuwasilisha
nyaraka mbalimbali za shindano lake hususan mikataba ya washiriki. Tatu
kutumia mawakala wasiosajiliwa na kupewa vibali vya BASATA.
Miongoni
mjwa mapungufu ambayo Kampuni ya LINO imeyafanyia kazi ni kuanza
mchakato wa usajili wa mawakala – BASATA na kufanyia marekebisho kanuni
na taratibu za uendeshaji wa Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania.
Aidha, LINO imewasilisha muundo wa kamati ya uendeshaji wa shindano
yenye muelekeo wa kuzingatia jinsia.
Katika kuboresha na
kurudisha hadhi ya shindano la Miss Tanzania, LINO International Agency
Limited imepewa kibali cha muda kisichozidi miezi minne (4) kwa ajili ya
maandalizi ya awali ikiwemo kukamilisha usajili wa mawakala katika
ngazi zote husika.
BASATA linapenda kuwafahamisha wadau wote wa
Sanaa hususan wale wa shindano la urembo la Miss Tanzania kwamba Kampuni
ya LINO imetekeleza maagizo ya msingi iliyopewa kama masharti ya
kufunguliwa. Na kwamba baada ya kufanyia kazi changamoto zilizokuwa
zimejitokeza BASATA limeyafungulia mashindano ya Miss Tanzania kwa
masharti ya kukamilisha changamoto zilizobakia.
Ni matarajio ya
BASATA kwamba kampuni ya LINO itazingatia taratibu zote za uendeshaji wa
matukio ya Sanaa nchini na kwamba haitarudia tena makosa
yatakayopelekea kuliweka shindano hili katika hali ya kushuka hadhi na
kuzua sintofahamu katika jamii.
Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJ
No comments:
Post a Comment