Yamekuwa hayo? Aliyewahi kuwa mwandani wa staa wa Bongo Fleva Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’, Penniel Mwingilwa `DVJ Penny’ amegoma kuulizwa
chochote kuhusu kitendo cha zilipendwa wake huyo kupata mtoto wakati
yeye alidaiwa kukataa kumzalia.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda,
wikiendi iliyopita, Penny alifunguka kwamba, haoni kama kuna sababu ya
kumzungumzia Diamond na mtoto wake (Tiffah) kwani walishaachana zaidi ya
miaka miwili sasa.
“Jamani, huyo mtu kwa sasa hanihusu na
sioni kama kuna sababu ya kumuongelea mtoto wake, anayepaswa kuulizwa
mambo ya Diamond ni Zari, kwa hilo mnisamehe (no comments), nikiulizwa
niulizwe mambo yangu tu,” alisema Penny.
GPL
No comments:
Post a Comment