Polisi
mjini Mwanga, mkoani Kilimanjaro umezuia msafara wa mgombea urais
kupitia Chadema, Edward Lowassa uliokuwa unaelekea Usangi kuhudhuria
mazishi ya kada wa CCM, Peter Kisumo.
Vyanzo
vya kuaminika toka mjini Mwanga vinasema, polisi walizuia msafara huo
kutokana na kujumuisha idadi kubwa ya magari ya viongozi waandamizi wa
Ukawa na wabunge wanaounda umoja huo jambo ambalo polisi hawakuafiki.
Taarifa
zinasema, tukio hilo lililotokea katikati ya Mwanga na Usangi lilizusha
mjadala wa zaidi ya dakika 30, polisi wakitaka Lowassa aende mazishini
peke yake huku magari mengine yaliyoambatana naye yarejee yalikotoka
jambo ambalo halikuafikiwa na mwanasiasa huyo.
Polisi wakiwa tayari kwa lolote baada ya kuzuia msafara wa LOWASSA |
No comments:
Post a Comment