Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amesema baadhi ya
kauli zinazotolewa na Umoja wa Vyama vya Upinzani (Ukawa), zinaashiria
uvunjifu wa amani pindi matokeo ya kura yatakapoanishwa baada ya zoezi
la upigaji kura Oktoba 25 mwaka huu.
Rais Kikwete alisema baadhi ya
kauli hizo zimekuwa zikionyesha wazi viashiria vya uvunjifu wa amani na
upotoshaji kwa kundi kubwa la vijana ambao wanapiga kura kwa mara ya
kwanza.
Akizungumza wakati akizindua Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao jijini Dar es Salaam Rais Kikwete alisema;
“Wamediriki
kusema wazi bila kificho kwamba patakuwa hapatoshi, hizi ni kauli
zinazoashiria uvunjifu wa amani. Tunachokisema CCM ushindi kwetu ni
lazima na tutashinda kwa kishindo na kwenda nginja nginja mpaka Ikulu.”
Kikwete
alisema CCM imejipanga kuhakikisha inapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu
ujao na kuongeza kuwa ili kufanikisha hilo wamepanga kikosi kazi
ambacho kitatembea nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, mtu kwa mtu
ikiwa kwa sasa tayari wameshaanza kufanya kampeni zao kupitia mtandao ya
simu za mkononi.
Katika hafla hiyo ya kuzindua kampeni hiyo
inayoratibiwa na msanii wa filamu na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema
Sepetu, Rais Kikwete aliwataka wanawake kaungalia mazuri yote
yaliyofanywa na Serikali ya CCM katika kumuinua mwanamke.
No comments:
Post a Comment