Staa mkongwe wa muziki kutoka DR Congo, Jenerali Defao baada ya
kutosikika kwa muda mrefu ameonekana huko Kenya, akiwa na muonekano
tofauti na alivyozoeleka kutokana na kupungua mwili kwa kiasi kikubwa,
na weupe wa ngozi yake ukitia mashaka.
Defao ambaye hata hivyo
haijajulikana rasmi ni shughuli gani imempeleka huko Kenya, kutokana na
muonekano huo, hisia za wengi zimetafsiri kuyumba kisanaa na kiafya kwa
msanii huyo aliyewahi kuwa gumzo kwa sanaa yake katika bara la Afrika na
Ulaya.
Hata hivyo, kuyumba kwa msanii huyo pia kunahusisha na
kupungua kwa mvuto wa aina ya muziki wa dansi kutoka DR Congo ambao
ulifanya vizuri sana katika miaka ya nyuma.
No comments:
Post a Comment