Zaidi ya wanachama 500 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) wakiwemo viongozi wa kata mbalimbali katika wilaya ya Ludewa
mkoani Njombe, wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha
ACT-Wazalendo.
Wanachama hao wamefikia maamuzi ya kukihama chama
hicho huku wakiwalalamikia viongozi wao wa CHADEMA wilaya na taifa
kumkata mgombea wao wa ubunge jimbo la Ludewa waliyemuhitaji Bwana Okol
Haule na kumuweka mgombea wanayemuhitaji wao bwana Bathoromeo Mkinga.
No comments:
Post a Comment