Serikali ya Somalia imepiga marufuku sherehe za kuadhimisha sikukuu ya Krismasi katika mji mkuu wa Mogadishu.
Mkurugenzi
mkuu katika wizara ya maswala ya dini,Sheikh Mohamed Khayrow, ameonya
kuwa maadhimisho kama hayo yasiyofungamana na dini ya kiislamu yanaweza
kusababisha mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa Al Shabab.''Maafisa wote wa kulinda usalama wanapaswa kusimamisha ama kuvunja mikutano ya aina yeyote yenye nia ya kuadhimisha sikukuu hiyo isiofungamana na dini ya Kiislamu.'' alisema Sheikh Mohamed
Mwaka uliopita wapiganaji wa Al shabab walishambulia kambi ya majeshi ya muungano wa Afrika AU iliyoko mogadishu wakati wanajeshi hao walikuwa wakisherehekea sikukuu ya Krismasi.
Wanajeshi 5 waliuawa katika shambulizi hilo la kuvizia.
Asilimia kubwa ya raia wa Somalia ni wasilamu.
No comments:
Post a Comment