Habari ya mjini kwa sasa ni mtoto mzuri Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwania Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini nyuma yake kuna habari zinazodai kuwa mrembo huyo ameingiwa na hofu ya kukatwa jina kama ilivyotokea kwa Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliyekuwa mmoja wa watia nia ya kugombea urais, Amani lina mkanda kamili.
Lowassa alikuwa miongoni mwa makada 33 kati ya 38 walioenguliwa na
Kamati ya Maadili ambayo ilipitisha majina matano pekee katika kikao cha
Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na baadaye Mkutano Mkuu kupitisha Mbunge wa
Chato, Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kwa Tiketi ya CCM.
Chanzo kilicho karibu na staa huyo kimepenyeza ‘ubuyu’ kuwa, Wema ambaye
anashikilia Taji la Miss Tanzania 2006/07, ameingiwa na hofu hiyo baada
ya kuona Lowassa ambaye ana sifa ya kukubalika kama alivyo yeye
ameenguliwa na kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM.
“Bibie (Wema) anajiamini, anakubalika kweli lakini kitendo cha Lowassa
ambaye alikuwa anaonekana kukubalika kimemtia hofu na kuona kumbe
kukubalika pekee si silaha ya ‘kuwini’ kupitishwa na chama,” kilisema
chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kwenda mbali zaidi kwa kudai hofu hiyo iliongezeka
kwa Madam hususan baada ya kusambaa kwa kuwepo kwa watu wasiompenda
kupandikiza chuki kwamba baadhi ya skendo zilizomgusa zinaweza
kumpotezea sifa ya jina lake kupitishwa na Halmashauri Kuu ya chama
chake.
“Si unajua tena Madam kwenye maisha yake ya sanaa amepitia skendo za
hapa na pale, hiyo inaweza kuchangia kumtia hofu maana wabaya wake
wanaweza kuitumia kama silaha hivyo amekuwa akitoa chozi na kumuomba
Mungu amfanikishe,” kilisema chanzo hicho.
Duru mbalimbali za habari zinaonesha kwamba kitu kikubwa kinachoangaliwa
kwa kiongozi ni suala la uwajibikiaji na si tabia binafsi au skendo.
Wapo viongozi ambao walikuwa na skendo lakini wameweza kupitishwa na
wananchi wao na kuwatumikia vizuri kuliko hata wale walionekana wasafi.
“Si kweli kwamba skendo ndiyo kigezo kikuu cha kumpitisha mgombea, mbona
watu kama akina Mike Sonko (alikuwa Mbunge wa Kenya), marehemu Amina
Chifupa (alikuwa Mbunge Viti Maalum, Vladimir Vladimirovic Putin (rais
wa urusi) na wengine wengi, walikuwa au walipata skendo lakini walifanya
vizuri katika uongozi wao,” alisema mwanaharakati mkubwa wa siasa
nchini aliyeomba hifadhi ya jina.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa kama kuna
uwezekano wa kumuengua mgombea yeyote kutokana na skendo au chuki
zinazoezwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho, alisema si kweli bali
wao wanafuata taratibu na kanuni walizojiwekea na si vinginevyo.
“Sisi tuna kanuni na taratibu za chama, hiyo ndiyo misingi yetu.
Hatumuengui mtu kwa chuki binafsi wala kitu kingine chochote zaidi ya
kufuata kanuni zetu,” alisema Nape.
Akizungumza na mwanahabari wetu hivi karibuni, Wema alikiri kupata hofu
hiyo kwa muda lakini ameshajiamini kutokana na kumuomba Mungu ambaye
amekuwa akimtanguliza katika kila jambo analolifanya.
“Kusema kweli mtu unapotaka kufanya jambo unapaswa kujiamini, hata mimi
mwanzo nilikuwa nimejipa matumaini ya hali ya juu kwamba Lowassa
atapita, lakini bahati mbaya akakatwa, naamini Mungu yupo, mimi naswali
usiku na mchana, Mungu atanisimamia katika hili,” alisema Wema.
No comments:
Post a Comment