Mafahari wawili Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Wema Sepetu ‘Madam’ wamezidi ‘kusherehesha’ bifu lao baada ya kupigana vikumbo kwenye mgahawa unaojulikana kama Snow Cream na kuchuniana kama vile hawajuani.
Kwa mujibu wa gazeti la Risasi,
Wema ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia kwenye mgahawa huo na wapambe
wake kisha baada ya muda kidogo kupita, Aunt pamoja na watu wengine nao
walifika na kukaa meza nyingine.
Habari zinadai kuwa baada ya Aunt kukaa, walitupiana macho na
Wema bila kupeana salamu ingawa Wema hakuwahi kumuona mtoto wa Aunt
tangu ajifungue.
Inadaiwa kuwa baada ya Aunt kumaliza
kula Ice Cream na kundi lake, waliinuka na kuondoka zao na kumuacha Wema
na marafiki zake.
Alipotafutwa Aunt ili aweze
kuzungumzia kitendo hicho na bifu lao lisema;
“Jamani unajua kila mtu alienda kwa ajili ya kazi zake na ndiyo kama
tulivyokutana kila mmoja alikuwa yupo na taratibu zake, sioni kama ni
bifu, sina comment,” .
No comments:
Post a Comment