Kokomaster amesema kuwa toka walipokutana na Diamond walizungumza na
kukubaliana kufanya collabo lakini amekuwa akimpiga chenga mpaka sasa.
Star huyo ambaye aliibuka na tuzo ya ‘MAMA Evolution’ katika MTV MAMA
2015, ameongeza kuwa kabla mwaka huu haujaisha anaamini collabo hiyo
itakuwa tayari imefanyika.
Diamond ametoa sababu za kuchelewa kufanya collabo na D’Banj.
“Tulikutana kule kwenye Do Agric tukafanya Cocoa na Chocolate,
tukatakiwa kufanya nyimbo ya mimi na yeye lakini nikaogopa ukianza na
msanii mkubwa sana itakuwa kurudi tena itakuwa tabu lazima uanze kwa
ngazi kwa ngazi kwa ngazi ili kesho na kesho kutwa ukitoa nyimbo
uonekane unazidi kupanda, sio unafanya nyimbo na mkubwa halafu kesho
unashuka, nafikiri ndio ikawa sababu pia nyimbo yangu ya kwanza sikuweza
kufanya na yeye ya kwanza.”
No comments:
Post a Comment