Rais
Barrack Obama na wanawe Sasha na Malia. Afisa mmoja wa chama cha
Republican amewakosoa mavazi yao.Watoto wa rais wa Marekani Barrack
Obama, Sasha na Malia wameshtumiwa kwa kukosa heshima na afisa mmoja wa
chama cha Republican baada ya kuhudhuria sherehe za kutoa shukrani.
Elizabeth
Lauten ,ambaye ni mkurugenzi wa mawasiliano wa mbunge Stephen Fincher
alitoa matamshi yake katika mtandao wa facebook ambayo baadaye
yalifutwa.
Aliku akikosoa sketi fupi zilizovaliwa na wasichana hao wa Obama.Bi
Lauteni pia aliwashtumu wasichana hao kwa kuonyesha uchovu wakati
waliposimama na baba yao katika sherehe hiyo ya ikulu ya Whitehouse.
Watoto wa Obama Sasha na Malia, wamekosolewa kwa mavazi yao.Maandishi yake yalisoma:
''Kwa wapendwa Sasha na Malia: najua kwamba bado mko katika usichana
wenu lakini ninyi ni miongoni mwa familia ya kwanza ya taifa hili,
tafadhali jaribuni kuwa na heshima.Tafadhalini jaribu kuheshimu jukumu
mlilopewa.
''Mama yenu na baba yenu hawaheshimu nyadhifa zao kama inavyohitajika na taifa kwa jumla.
Kwa hivyo naona kwamba mnakosa ile hadhi ya kuwa kioo cha jamii.
Maandishi hayo yaliendelea na kuwashauri wasichana hao kuonyesha kwamba wanaishi katika ikulu ya Whitehouse.
No comments:
Post a Comment