Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imewahukumu kifungo cha miaka
mitatu jela aliyekuwa Waziri wa Fedha Basil Mramba na aliyekuwa Waziri
wa Nishati na Madini Daniel Yona. Licha ya kuhukumiwa miaka 3 jela
Mawaziri hao wa zamani wanapaswa kulipa faini ya Sh 5m kila mmoja
Katika kesi hiyo ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia hasara
serikali, mtuhumiwa mwingine aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha,
Gray Mgonja amekutwa hana hatia.
No comments:
Post a Comment